Children’s’ Book Review: Sungura Mjanja

Na Gloria Mwaniga

Kichwa : Sungura Mjanja
Muandishi : Rebecca Nandwa
Mchapishji: Jommo Kenyatta Foundation

Sungura ni mwana wa kipekee wa wazazi wake. Mama na baba yake wanajitahidi vilivyo ili wamfunze mwanao tabia nzuri. Anapoendelea kuwa mkubwa, wazaziwe wanamfunza kazi zote za kinyumbani na kumuhimiza kutia bidii za mchwa maishani mwake.
Siku moja, babake sungura alienda safarini , mamake akashikwa na ugonjwa wa kifua na kulazwa.Basi ilimbidi sungura aende shambani kulima na kupanda njugu kwa niaba ya wazaziwe.

Je sungura ataweza kulima shamba hilo lote na kupanda mimea?
Je kila alfajiri aondokapo na jembe begani na redio mkonono, sungura huenda kulima au kucheza?
Na je ,ikiwa asante ya punda ni mateke, basi hasira ya punda ni nini?

Katika hadithi hii ya kuburudisha , kuelekeza na kuchekesha , Mwandishi Rebecca Nandwa ameweza kuwapatia wanafunzi wa madarasa ya juu katika shule za msingi funzo la busara kuhusu umuhimu wa bidii na uaminifu maishani.
Picha nzuri za kuwafurahisha watoto na kupendeza zaongezea uzuri wa hadithi hii kwa watoto.

Kitabu hiki chapatikana kwa maduka ya kuuza vitabu kote nchini .

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s